Akitoa mada katika kongamano la kielimu lililofanyika katika Chuo cha Jamiatul Mustafa (s) Jijini Dar es Salaam - Tanzania, Sheikh Dr.Raihan alisisitiza kuwa funga za viungo ni njia muhimu ya kufikia taqwa, kuimarisha nidhamu ya nafsi na kukuza maadili ya kijamii miongoni mwa waumini.

21 Februari 2026 - 15:03

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kongamano la kielimu lenye anuani “Funga za Viungo zinatupeleka katika Taq'wa” limefanyika Jumamosi tarehe 21/02/2026 katika Chuo cha Al-Mustafa International Foundation- Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na walimu, wanafunzi wa dini pamoja na waumini mbalimbali waliopenda maarifa ya Kiislamu. Mzungumzaji mkuu, Sheikh Dr. Raihan Yasin, alieleza nafasi ya Funga za Viungo (Macho, Mikono, Miguu, n.k...) katika kujenga nafsi na kuimarisha Ucha_Mungu (tatqwa).

Akinukuu mafundisho ya Qur’ani Tukufu, alisisitiza kuwa lengo la funga ni kumfanya mwanadamu awe na Taq'wa, na kwamba funga za sunna ni mwendelezo wa mafunzo ya kiroho hata baada ya kutekeleza funga ya faradhi ya Ramadhani.

Sheikh Dr. Raihan Yasin alibainisha kuwa funga za Viungo vya mwili humfundisha mtu nidhamu, subira na kujidhibiti, pamoja na kuimarisha mshikamano wa kijamii kwa kuwafanya watu wahisi hali ya wahitaji na kuongeza moyo wa kusaidiana.

Mwisho wa kongamano hilo, washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kubadilishana mawazo kuhusu namna bora ya kutekeleza funga za Viungo katika maisha ya kila siku.

Kongamano hilo ni sehemu ya mfululizo wa programu za kielimu na kiutamaduni zinazoandaliwa na chuo hicho nchini Tanzania.

Your Comment

You are replying to: .
captcha